BAADA ya Yanga kupata uongozi mpya ambao upo chini ya Mwenyekiti, Mshindo Msolla na Makamu wake Frederick Mwakalebela wameongeza nguvu ya viongozi wengine wawili huku wakiwa na mpango wa kuongeza mjumbe mmoja baadaye.
Wanachama hao ambao wameongezwa kwenye nafasi na Kamati ya Utendaji kwa kutumia mamlaka iliyopewa na Ibara ya 28 (1) (d) ya Katiba ya Yanga ya mwaka 2010, imefanya uteuzi wa wanachama wafuatao kuwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga:-
Dkt Athumani Kihamia, Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Shija Richard Shija, Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Uteuzi huo unaanza mara moja.
Katiba hiyo imetoa mamlaka kwa Kamati ya Utendaji ya Yanga kufanya uteuzi wa wajumbe watatu wa Kamati ya Utendaji hivyo huyo mmoja aliyebaki kamati imesema itamteua baadaye.
Kwahiyo michango itaitimishwa lini? Kwahiyo tarehe 18 siyo kuchangishana? Je, baada ya sikukuu ya iddi harambee itafanyika lini? Hamuoni sababu za kuahirisha hazina mantiki kwakuwa wakati wa sikukuu matumizi ya fedha ni mengi watu wanatumia fedha kwa ajili ya sikukuu kwa familia zao...hili hamjalifikiria? Au mngesema waliothibitisha kushiriki harambee ya awali ya tarehe 18 watashindwa kuhudhuria? Je, hamuoni kuwa harambee ikifanyika baada ya ligi kumalizika mtakuwa mmechelewa kwani timu nyingi zitakuwa likizo wachezaji wengi watakuwa hawapo na timu za taifa zitakuwa kwenye kambi za maandalizi ya Afcon?
ReplyDeleteUshauri
Kamati ya Usajili itakayoundwa ihusishe wanasheria, madaktari, na makocha au wachezaji wa zamani pamoja na wenye uwezo wa kifedha.
1. Maoni Kuhusu zoezi la Kuchangia Yanga----Mikoa Mingine mfano Mwanza, Kagera, Mara, Shinyanga nk. (Kanda ya Ziwa) au Kanda za Nyanda za Juu Kusini (Mbeya, Iringa, Rukwa,) na Mikoa ya Kusini NAZO ZIFANYE FUNDRAISING DINNER OR GALA KUCHANGIA KLABU KABLA YA MWISHO WA JUNE....PESA ITAKAYOPATIKANA IINGIE KWENYE ACCOUNT YA KLABU KWA MATUMIZI YALIYOKUSUDIWA (USAJILI NA MISHAHARA YA WACHEZAJI, BENCHI LA UFUNDI NA WAFANYAKAZI WA KLABU.....
ReplyDelete2. BAADA YA HAPO UTARATIBU WA MICHANGO USITISHWE RASMI MWEZI JULY 2019....ISIPOKUWA ADA ZA UANACHAMA NA ILI LIENDANE NA KUINGIZA WANACHAMA WAPYA
Ahsante