May 20, 2019


KUONDOKA kwa nahodha wa timu ya Manchester City, Vincent Kompany kumewagusa wachezaji wa timu yake hiyo ya zamani kutokana na mchango wake alipokuwa ndani ya kikosi hicho baada ya kuvaa kitambaa hicho kwa muda wa miaka nane.
Kompany ameondoka City baada ya masaa 24 kupita kwa kikosi chake kutwaa ubingwa wa kombe la FA kwa mabao 6-0 dhidi ya Watford, siku ya Jumamosi na tayari aliongoza kikosi hicho kutwaa mataji mawili ambayo ni pamoja na Carabao na lile la Ligi Kuu England.
Wachezaji wa City wamesema kuwa Kompany ambaye anakwenda kuwa kocha mchezaji wa kikosi cha Anderlecht  alikuwa na mchango mkubwa ndani ya kikosi hicho tangu ajiunge mwaka 2008 akitokea Hamburg.
Mshambuliaji mbunifu Bernardo Silva ametupia picha zake kwenye mitando ya kijamii akiwa amevaa nguo zenye rangi nyeusi ikiwa ni ishara ya huzuni kwa kuondoka kwa nahodha huyo kwenye kikosi hicho.
Meneja wa City, Pep Guardiola amesema kuwa watamkosa mchezaji mwenye juhudi na kipaji cha uongozi muda wote ndani ya uwanja.
"Muda ambao Kompany akiwa fiti ndani ya uwanja ni lazima utampenda kwani anafanya kazi yake ipasavyo kuiongoza timu kufuata utaratibu ila kwa bahati mbaya ameamua kuondoka.
'Joe Hart, Vincent Kompany, Sergio Aguero, Yaya Toure na David Silva wametusaidia sana msimu huu kupambana kufanya vizuri," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic