May 20, 2019

KATIBU Mkuu wa Singida United, Festo Sanga amesema kuwa wapinzani wao Simba wanapaswa watambue kwamba Namfua sio sehemu ya kutangaziwa ubingwa hivyo hilo walisahau.

Sanga amesema kuwa nafasi waliyopo kwa sasa Singida United sio salama kwa kuwa timu nyingi zimetofautiana kwa pointi chache hivyo ni lazima wapambane kupata pointi tatu.

"Kwenye msimamo tupo nafasi ya tisa ila kwetu sio salama, tunajua kwamba Simba wanahitaji pointi mbili ili kutangazwa ubingwa, nasi tunasema Namfua sio sehemu ya Simba kutangazwa kuwa mabingwa.

"Tumewekeza kwa ajili ya kushinda mchezo wetu, utakuwa mchezo wa jasho na damu pia tunatambua kwamba utakuwa mchezo wetu wa mwisho kucheza uwanja wa Namfua, lazima apigwe tu licha ya kwamba tunamheshimu.

"Tumejipanga kuona kwamba Simba anataga mayai matatu ikiwa na maana anaacha pointi tatu uwanja wa Namfua kivyovyote vile lazima akae uwanja wa Namfua kwa kuwa hatupo sehemu salama," amesema Sanga.

Singida United imecheza michezo 36 imejikusanyia pointi 45 wakati wapinzani wao Simba wapo nafasi ya kwanza wakiwa wamecheza michezo 35 wamejewekea kibindoni pointi 88.

3 COMMENTS:

  1. Tukutane kesho saa 18:00 baada ya gem mkuu

    ReplyDelete
  2. wamesema sana maneno hayo wenzako

    ReplyDelete
  3. Simba ilihitaji kutoka sare kesho iate pointi moja na kutangaza ubingwa lakini baada ya kusikia kiongozi wa Singida akitamka maneno haya sasa kesho kazi tu Simba wekeni full mziki tuwatandike hawa goli 3 - 0 tunao huo uwezo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic