Na George Mganga
Bwire asiyeishiwa maneno ametamba kuwa ni lazima waimalize Yanga leo katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa majira ya saa 10 kamili za jioni.
Ameeleza kuwa katika mchezo uliopita dhidi ya Lipuli waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 na akisema mechi hiyo ilikuwa ni ya mazoezi kwao.
Kufuatia ushindi huo, Bwire amefunguka kuwa waliwafunga wababe wa Yanga hivyo haitakuwa na ugumu wowote wa kuwafunga Yanga.
"Sisi tunataka alama tatu tu na si kingine.
"Kama tuliwafunga Lipuli ambao ni wababe wa Yanga, kwanini wao tuwashindwe, si itakuwa kazi rahisi tu.
"Kikosi chetu ni kama Barcelona, tunapiga mwingi na uhakika wa kupata alama upo." amesema.
Yanga inawakaribisha Ruvu Shooting iliyo nafasi ya 14 ikiwa na alama 42 wakati Yanga iliyo nafasi ya pili in alama 80.
Unadhani matokeo yatakuwa ya aina gani? Tupe utabri wako kwa kudondosha komenti yako hapo chini
Naona yanga anaenda kufa 0-1 au iwe duro lakini sioni kama yanga atashinda
ReplyDeleteFt 0-0
ReplyDeleteYanga anashinda 1 bila
ReplyDeleteRuvu ndo wenyeji mchezo huu. (Ruvu 1 - Yanga 0).
ReplyDelete