May 15, 2019


KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa hana presha na suala la kubeba ubingwa kwani amewapa kazi mpya wachezaji wake ya kutafuta mabao kwenye kila mchezo.

Aussems amesema kuwa wachezaji wake wanashindwa kuwa makini wanapofika eneo la hatari tatizo ambalo lilikuwa limeanza kupata dawa ila limejirudia kutokana na uchovu.

Akizungumza na Saleh Jembe, Aussems amesema kuwa kwa sasa wamekuwa na michezo mingi ambayo ipo karibu hali inayomfanya abadili kikosi chake cha ushindi mara kwa mara.

"Unajua nina michezo mingi migumu tena ipo karibu sasa hapo inakuwa ngumu kubaki na kikosi kimoja wakati wote ni lazima wengine wapumzike hivyo inakuwa ngumu kuwa na kikosi kimoja.

"Kwa sasa tatizo la umakini kwa wachezaji limeanza kujirudia ila najua sababu ni uchovu, bado tuna nafasi ya kufanya vizuri na kutimiza lengo letu la kutwaa ubingwa," amesema Aussems.

Simba ipo nafasi ya pili baada ya kucheza michezo 33 imebakiwa na michezo mitano ili kukamilisha mzunguko wa pili msimu huu.

1 COMMENTS:

  1. Yes coach nani anaweza kutuzuiya??.Sisi ndio mabingwa wa Tanzania

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic