KOCHA Mkuu wa Yanga amesema kuwa hatanyamaza kuzungumza juu ya kuonewa kwake na timu yake kila inapotokea akishinda ama akishindwa kwa kuwa hakuna atakayemzuia kufanya hivyo hata iwe Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) mpaka mambo yatakapokuwa sawa.
Zahera amesema kuwa anaheshimu mamlaka zote zilizopo kutokana na kazi ambazo zinafanya ila pale ambapo anaona haki haitendeki ni lazima azungumze bila kuogopa.
"Niliitwa na TFF, nimekwenda kuonana nao wameniambia mambo yao nimewaskiliza, sasa hata kama nimeitwa haimanishi nitanyamaza pale ambapo mambo yanakuwa hayaendi sawa lazima niseme sitanyamaza.
"Mpira wetu ili uendelee ni lazima makosa yafanyiwe kazi, kama tutakuwa tunanyamaza nani atatusemea, Yanga ikishindwa kupata matokeo tunaumia hivyo tunasema ili makosa yafanyiwe kazi," amesem Zahera.
atawasemea Manara
ReplyDeleteZahera kwa Yanga hii unamaanisha haiwezi kufungwa na timu yoyote ile? hapa Tanzanzia maana nimekwisha fatilia mahojiano yake huyu zahera akifungwa kuna mambo mawili 1. lawama kwa Tff na Marefaree 2. Haitaji ubingwa kavuka lengo. Akifunga anasema nitapambana mpaka hatua za mwisho hapo ndo utajua proffesional coach, maana mazuri sawa mabaya kwake ni sumu.
ReplyDelete