MILIONI 70 ZAMPELEKA MTANZANIA BOTSWANA USAKATA KABUMBU
Kiungo Mtanzania, Abdallah Hamisi ameondoka klabu ya Bandari ya Kenya kuelekea nchini Bostwana.
Abdallah ameondoka kwa ajili ya kwenda kujiunga na klabu ya Orapa United ya Botswana kwa mkataba wa miaka miwili.
Imetajwa kuwa dau la shilingi za Tanzania milioni 70 limeelezwa kutumika kwa ajili ya uhamisho wa mchezaji huyo.
Tayari Bandari wameshamalizana na Oarapa juu ya mchezaji huyo ambaye alikuwa moja ya nguzo muhimu ndani ya timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Kenya.
0 COMMENTS:
Post a Comment