NAHODHA Msaidizi wa Simba, Mohamed Hussein 'Tshabalala' amewaomba radhi mashabiki wa Simba kwa kitendo chake cha kujifunga mwenyewe kwenye mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar ambapo bao hilo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo.
Tshabalala alijifunga bao hilo akimalizia pasi iliyopigwa na nahodha wa Kagera Sugar, Paul Ngalyoma kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Uhuru.
"Haikuwa malengo yangu kufanya hivyo ni sehemu ya mpira, kwa sasa tunachotakiwa ni kupambana kwa ajili ya michezo yetu ijayo ili kupata pointi tatu muhimu, bado tuna nafasi ya kufanya vizuri," amesema Tshabalala.
Ushindi huo kwa Kagera umewatoa nafasi ya 12 waliyokuwa awali mpaka nafasi ya tisa baada ya kujikusanyia pointi 43 huku Simba ikisalia nafasi ya kwanza na pointi zake 81.
0 COMMENTS:
Post a Comment