May 15, 2019


BAADA ya kikosi cha Namungo FC chenye maskani yake Lindi kupanda Darakja kutoka Ligi Daraja la kwanza mpaka Ligi Kuu Bara, kimewatumia ujumbe vigogo wa ligi Simba na Yanga.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Namungo, Kidamba Namlia amesema kuwa walijipanga kupanda ndio maana wamefanikiwa hivyo hawatakuwa na hofu ya kushiriki ligi msimu wao wa kwanza.

"Tumejipanga ndio maana tumepanda Daraja, ni wakati wetu sasa kuonyesha kwamba hatukubahatisha kupanda  hivyo hao wanaojiita vigogo wasitarajie kupata mteremko hapa.

"Iwe Simba iwe Yanga hatuna hofu nazo kwa kuwa zote tumecheza nazo na hakuna kikosi ambacho kimebahatika kupata matokeo kiwepesi tuliwapa taabu kidogo ndo wakatuzidi hivyo kwa kuwa tumepanda tutawakomalia wote mwanzo mwisho," amesema Namlia.

Katika michezo yote ya kirafiki ambayo Namungo walicheza na Simba na Yanga walitoshana nguvu, ila kwenye mchezo wa kombe la FA, Yanga ilishinda bao 1-0 mkoani Lindi.


1 COMMENTS:

  1. Hiyo lugha sidhani kama ni kimwera,kiyao,kimatumbi au kimakonde.......nadhani itakuwa ni Ki Indonesia

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic