UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa bado unaendelea kuzungumza na mshambuliaji wao Obrey Chirwa ili aweze kuongeza mkataba kuendelea kuitumikia timu hiyo.
Chirwa alisajiliwa na Azam FC msimu huu ambapo mkataba wake unakamilika mwisho wa msimu huu hali liyofanya viongozi kuendelea kuzungumza naye ili aongeze mkataba.
Akizungumza na Saleh Jembe, mratibu wa Azam FC, Philip Alando amesema kuwa wamejipanga kufanya usajili makini msimu ujao na tayari wamefikia sehemu nzuri ya mazungumzo na Chirwa mpaka sasa.
"Kwa sasa tumefikia sehemu nzuri ya mazungumzo na mchezaji wetu Chirwa kwani tunahitaji kupata huduma yake ndani ya kikosi chetu msimu ujao kutokana na kuonyesha uwezo ambao unaridhisha, " amesema Alando.
Chirwa amefunga mabao matatu mpaka sasa kwenye ligi na ametoa pasi moja ya bao tangu alipojiunga na Azam FC kwenye michezo ya ligi.
0 COMMENTS:
Post a Comment