NDEMLA KUSAINI YANGA
KIUNGO wa Simba, Said Ndemla, ametoa msimamo wake akisema kuwa hana haraka ya kusaini klabuni hapo kwa kuwa anataka kucheza nje ya nchi, lakini akasisitiza ikishindikana nje hata Yanga yupo tayari kusaini.
Katika msimu huu, Ndemla alipewa ruhusa na Simba ya kwenda kufanya majaribio katika timu ya Eskilstuna ya Sweden, ambapo hadi sasa majibu yake kama alifuzu au la yalibaki kuwa kitendawili.
Ndemla alisema pamoja na mkataba wake kufikia ukingoni mwishoni mwa msimu huu, hana haraka ya kuongeza mpya, hadi hapo dili lake la kwenda kucheza nje ya nchi litakaposhindikana.
“Sina mpango wa kusaini Simba mapema hii, zaidi najipanga kuangalia dili langu la kucheza nje ya nchi, endapo nitakwama basi nitakuwa tayari kusaini Yanga au kuongeza mkataba Simba kama watakuwa bado wanahitaji huduma yangu.
“Tetesi zote ambazo zimekuwa zikisemwa juu yangu naweza kusema zitabaki kuwa tetesi ila mipango kamili naijua mwenyewe, japo nasikia kuna watu wanazusha eti kuwa nilitolewa kambini kisa niligoma kusaini Simba, hilo si kweli, mimi ninaumwa sasa ni wiki nipo tu nyumbani naendelea na matibabu,” alisema Ndemla.
Bora Wende Yanga hayo maneno kuwa yanga inashindwa kulipa mishahara usisadiki Huko ndio utastarehe Roho yako kuliko kwenda nje ya nchi au kubaki simba wasiokupa nafasi. Kweli usifanye haraka ngoja mazuri Kwa yanga
ReplyDeleteYanga mtaweza kumununua Ndemla au ndo shamsham za usajili?
ReplyDeleteKipindi hiki ni cha kuuza magazeti ndiyo maana Bwana Yesu aliwaambia waandishi ole went.
ReplyDeleteKama Kuna mchezaji wa Simba anataka kwenda yanga wamwache aende tuna wachezaji wengi wenye uwezo
ReplyDeleteHuyu hata akienda sie hatupi shida.. kwani msimu huu amecheza mechi ngapi? Mpaka tumbabaikie.. kwangu mimi aondoke akapate nafasi ya kucheza mechi nyingi zaidi timu nyingine
ReplyDelete