YANGA WAMKOMALIA MO, WAAPA KUMCHOMOA MKUDE
SAKATA la usajili wa kiungo wa Simba, Jonas Mkude ambaye anamaliza mkataba wake na klabu hiyo hivi karibuni limeendelea kupamba moto na uongozi wa Yanga umedai kuwa unaendelea kupambana kuhakikisha unamchomoa mchezaji huyo klabuni hapo.
Unaambiwa kuwa licha ya hivi karibuni Mwekezaji Mkuu wa Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ kuwataka Wanasimba kutokuwa na wasiwasi kuwa Mkude haendi popote baada ya kufanya naye mazungumzo mara tu aliposikia kuwa timu hiyo imemtengea Sh milioni 120, mambo bado ni moto.
Habari za kuaminika ambazo Championi Jumatatu limezipata kutoka ndani ya Yanga zimedai kuwa uongozi wa timu hiyo bado unaendelea kupambana na Mo ili kuhakikisha unamchomoa Mkude katika kikosi hicho cha Simba ambacho ameanza kukitumikia tangu msimu wa 2011/12 baada ya kupandishwa kutoka kikosi cha vijana.
“Bado tunaendelea kupambana ili kuhakikisha tunamsajili Mkude kutoka Simba kwani licha ya kukutana na Mo hivi karibuni bado mambo kwa upande huo hayajakaa sawa.
“Fedha ambayo Mo anataka kumpatia haina tofauti kubwa na ile waliyompatia miaka miwili iliyopita wakati alipokuwa akisaini mkataba ambao unamalizika hivi karibuni na inavyoonekana hawapo tayari kumwongezea.
“Kwa hiyo, baada ya kuona hivyo tuliamua kumtafuta meneja wake ambaye pia ni mwanasheria wake na kuzungumza naye na bila kusita ametuambia kuwa kama kweli tunamtaka basi tutoe Sh milioni 120 sababu Simba fedha wanayotaka kumpatia ni kidogo,” kilisema chanzo hicho cha habari.
Alipoulizwa kuhusiana na hilo, Meneja wa Mkude ambaye aliomba kutotajwa jina lake gazetini, alisema: “Ni kweli kabisa ishu ya Mkude kuongeza mkataba mpya na Simba bado mambo hayajakaa sawa, kwani fedha wanayotaka kumpatia haina tofauti na ile ya miaka miwili iliyopita.
“Lakini pia Yanga bado nao tunaendelea kuzungumza nao, ila wao ofa yao kidogo ipo juu, ni nzuri, lakini nimewaambia waongeze kama kweli wanamtaka watoe Sh 120 milioni ambayo walikuwa wamemuahidi. Miaka yake nayo inazidi kwenda kwa hiyo hawezi kubaki Simba kwa sababu anaipenda tu huku akipata maslahi kidogo na kuacha kwenda kujiunga na timu ambayo imetoa fedha nyingi ambazo zitamwezesha kuitengeneza vizuri kesho yake.”
Wacheni. Mmeipata wapi hela ya kumkomoa Moo, au hiyo kimbia na bakuli. Jamaa wanachekesha Sana na vituko vyao
ReplyDeleteNgoja tusubiri maana utatoa fedha nyingi kumnunua mchezaji mmoja wakati wenzako wanapata fedha za CAF kufidia hapo halafu wewe baada ya muda mshahara unakosekana.
ReplyDeleteProtas-Iringa
Mie ni mwanasimba lkn nawahatadharisha viongozi wa Simba wasiingizwe chaka na wapigaji.Waacheni Yanga wamchukue kwa hilo dau la 120m na ni bora Simba igharamike kwa kumtafuta kiungo Mkabaji na centre back wenye nguvu na umbo la kutosha Kama kina Yaya Toure na hatuhitaji wachezaji wa kudokoa mipira... kumbukeni mechi ya Vita iliyochezwa Kinshasa wqlivyotufanyizia na mipira ya kona na cross jinsi beki zetu walivyoshindws kuicheza mipira hiyo.Wawa hana spidi na uwezo umepungua.Kama Simba tuko serious Mwacheni Mkude aende akachukue hiyo pesa ya Yanga na sie tutafute wachezaji wa kushindana na TP Mazembe ambayo nao imekataa kutoa dau zaidi alilotaka Ajib.
ReplyDeleteSimba wamwacue Mkude aende Hana thamanu anayotaka kupewa
ReplyDeleteMkude sio wa thamani ya milioni 120 tena hata miliomi 70 hastaili. Mwacheni aende zake tafuteni mtu mwenye uwezo wa kama Fabrice Ngoma aliyekuwa AS VITA
ReplyDeleteDah Mkude kama kweli Yanga wanawashwa na hiyo dau la 120m na wanaweka mezani kachukue haraka lkn Simba chonde msiingizwe choo cha kike kwani Mkude hana thamani hiyo labda sana sana mpeni 50m.Kuna wakata umeme wa kazi huko Zambia, Zimbabwe,DRC Congo kwa bei muafaka.Mkude wa sasa kisoka sio wa wakati ule na hajitumi...
ReplyDeleteMkude Nenda Baba Ukaone Wanavyoxhinda Njaa Ajib Ulimuona Xembuxe Wewe
ReplyDeleteMKUDE UNACHELEWA NENDA, 120ML NINI BWANA? UNAWEZA KUPEWA PESA KIDOGO LAKINI ANGALIA MWISHO WA MWAKA UMEVUNA BONUS KIASI GANI.YANGA WALISAJILI VIZURI KWA KUPITIA MANJI TATIZO WALILOLIPATA NI KUA, WALISHINDWA ,KUWAMUDU WACHEZAJI KWA MISHAHARA NA MAMBO MENGINE.TATIZO SI USAJILI.
ReplyDelete