May 28, 2019


UONGOZI wa Singida United umesema umejipanga kupata pointi tatu leo mbele ya Coastal Union utakaochezwa uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Leo Singida United inamaliza mchezo wake wa mwisho kwenye ligi msimu huu ikiwa Tanga mbele ya Coastal Union.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema hesabu kubwa ni kubaki kwenye ligi mengine yatafuata.

"Mchezo wetu wa leo tunahitaji pointi moja tu ili tubaki kwenye ligi,maandalizi ambayo tumeyafanya yapo vizuri na ni nafasi yetu yetu kubaki kwenye ligi na kujipanga upya kwa ajili ya msimu ujao," amesema Katemana.

Singida United ipo nafasi ya 11 ikiwa na pointi 45 baada ya kucheza michezo 37.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic