May 28, 2019

KOCHA wa Mbao FC, Salum Mayanga amesema kuwa leo wamejipanga kupata pointi tatu kwenye mchezo wao wa mwisho dhidi ya Kagera Sugar utakaochezwa uwanja wa CCM Kirumba.

Mbao ipo nafasi ya 13 baada ya kucheza michezo 37 imejikusanyia pointi 44 huku wapinzani wake Kagera Sugar wakiwa nafasi ya 17 baada ya kucheza michezo 37 wana pointi 43 kibindoni.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mayanga amesema kuwa malengo ya timu ni kubaki kwenye ligi na kitakachowapa nafasi ya kubaki msimu ujao ni ushindi tu.

"Hakuna njia nyingine ya sisi kubaki kwenye ligi zaidi ya kushinda, hivyo ni wakati wetu kufanya vizuri mchezo wetu wa mwisho mashabiki watupe sapoti," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic