May 10, 2019


SIMBA, juzi ilifanikiwa kuweka rekodi mpya katika Ligi Kuu Bara baada ya ushindi dhidi ya Coastal Union ya Tanga na kujikita kileleni mwa ligi hiyo.

Ushindi wa juzi wa mabao 8-1 dhidi ya Coastal ulifanya timu hiyo kujiwekea rekodi mpya katika ligi kuu ya kufikisha mabao 69 katika michezo 31.

Ikumbukwe kuwa msimu wa 2015/16 Simba walimaliza ligi wakiwa na mabao 45, msimu wa 2016/17 wakamaliza wakiwa na mabao 50 na msimu uliopita walifunga mabao 62.

Hivyo, kwa idadi ya mabao waliyonayo sasa wamefanikiwa kuvunja rekodi yao ya misimu kadhaa iliyopita.

Aidha, mara ya mwisho Simba kufunga mabao mengi katika mechi moja ilikuwa msimu uliopita katika mchezo wao dhidi ya Ruvu Shooting ambapo walishinda mabao 7-0.

Rekodi nyingine walizovunja Washambuliaji wa Simba Meddie Kagere, John Bocco na Emmanuel Okwi wote wamefunga zaidi ya mabao 10 ndani ya msimu mmoja.

Mastaa hao wamefunga hat trick tatu kati ya tano zilizofungwa msimu huu. Okwi ana mbili, Kagere ana moja.

Pia, Kagere na John Bocco wamebeba tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi mara mbili kila mmoja ingawa hawajamfunika Heritier Makambo wa Yanga aliyebeba mara tatu.

Rekodi nyingine ni pacha kali zaidi ligi kuu baada ya kufikisha mabao 48. Bocco ana mabao 14, Kagere (20) na Okwi (14).

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic