KUTOKANA na malalamiko ya Makocha wengi pamoja na viongozi kwenye mechi za lala salama kuhusu waamuzi, Chama Cha Waamuzi Tanzania kilicho chini ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kimesema kinafuatilia kwa hatua kila mechi na mwamuzi atakayebainika ana makosa adhabu kali itachukuliwa juu yake.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mwenyekiti wa Chama cha waamuzi, Salum Chama amesema kuwa waamuzi wote wanatakiwa watambue kwamba Chama hakilali na kinawafuatilia hatua kwa hatua.
"Kwa sasa ni muda wa lala salama, kumekuwa na malalamiko mengi ambayo tunayaskia, wapo pia ambao wanayaleta ofisini hivyo sisi tunachowataka waamuzi wawe makini na wafuate sheria 17 za mpira wakibainika wamekosea adhabu kali juu yao zitachukuliwa.
"Wengi tumekuwa tukikaa nao kuwakumbusha namna ya kuboresha mpira wetu na hawajui kama tunawafuatilia hatua kwa hatua jambo litakalosaidia tumalize ligi kwa amani, tuna mbinu nyingi ambazo tunazifanya ili kuona kwamba tunapata dawa ya hili tatizo ambalo linazidi kuwa sugu," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment