May 20, 2019


UONGOZI wa Simba umesema kuwa hamna namna yoyote ile kwa sasa kwa kikosi chao kwa michezo iliyobaki ni lazima washinde kwa kuwa wamejipanga.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa mchezo wao dhidi ya Singida United wamejipanga na wanahitaji pointi tatu muhimu.

"Tunatambua mchezo wetu dhidi ya Singida United utakuwa mgumu ila tunachokwenda kukifanya kwa michezo yetu iliyobaki ni kushinda tu, hivyo Singida United wajipange kwa hilo.

"Tunajua kwamba kuna matokeo matatu kwenye mpira ambayo ni sare, kufungwa na kutoka sare sisi yote hayo hatutambui hesabu zetu ni kushinda tu," amesema Manara.


3 COMMENTS:

  1. Si kwa maneno matupu tu bali Simba wanatakiwa kuwa na mikakati maalum ya kiushindi dhidi ya Singida la sivyo wataangukia pua. Singida ni timu kibaraka wa Yanga kwa kila namna. Ni tawi la Yanga na kama vile haitoshi Singida sasa inafundishwa na Fred Flex Minziro aliekuwa machezaji muandamizi wa Yanga na ni mwanachama wa Yanga pia hadi hivi tunavyozungumza. Ukiachana na Minziro kuna viongozi wakuu wa singida kama akina Mwigulu Mchemba ambae ni kiongozi wa Yanga pia mkoani singida na kama kuna timu kwenye ligi kuu bara amabazo Yanga walitegemea kuzitumia kuiharibia Simba kwenye safari yao ya ubingwa basi Singida United ni moja kati ya timu hizo. Kwa hivyo Simba mechi dhidi ya Singida lazima wachezaji wajiandae kwa vita hasa na sio maneno matupu ya msemaji wa Simba.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Naunga hoja iliyowasilisha.Hii mechi wachezaji waichukulie kama fainali na si ya kimchezo-mchezo ni ndio do or die game.Hii ndio mechi ya kutanganza ubingwa ili tuwaache jirani zetu wakitesekaa na kama vipi wajibebe

      Delete
    2. Umesema sahihi kabisa. Mwaka jana mechi na Kagera mbele ya Rais wa Nchi tulipigwa kwa kudharau mechi na baadae majibu rahisi tu mpira una matokeo 3. Kauli hizi zinakeraaa. Sisi tunataka ushindi tu hatutaki kudharau mechi. Singida ni Tawi la wapinzani wetu, lazima kuwapiga kisawasawa bila huruma, hata goli 4 - 0 inapendeza.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic