Searching...
Select a Page
  • MWANZO
  • KITAIFA
  • KIMATAIFA
  • MAKALA
  • BURUDANI
  • USAJILI
  • SALEHJEMBE TV
  • HABARI ZINGINE
    • TENNIS
    • GOLF
    • WWE
    • FOMULA ONE


Home » Kimataifa » SEVILLA KUTUA KESHO DAR, YALETWA NA SportPesa KUIVAA SIMBA
May 20, 2019

SEVILLA KUTUA KESHO DAR, YALETWA NA SportPesa KUIVAA SIMBA



TIMU ya Sevilla inatarajiwa kuwasili nchini Tanzania kesho Jumanne kwa ajili ya mchezo wa kirafiki ulioandaliwa na Kampuni ya SportPesa kwa ushirikiano wa La Liga.
Sevilla inatarajiwa kucheza mchezo huo wa kirafiki na Mabingwa wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Alhamisi ya wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam saa moja kamili usiku.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas amesema “SportPesa inakwenda kuweka historia kwa mara nyingine tena nchini kwenye sekta ya soka kwa kuileta timu ya kimataifa ya Sevilla.
“Kupitia ujio wa timu ya Sevilla watafanya shughuli mbalimbali zenye lengo la kuinua sekta ya michezo nchini kwa vijana na soka kwa ujumla.
“Watatoa mafunzo ambayo yatahudhuriwa na timu ya vijana ya Bom Bom FC kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar bila kusahau semina elekezi itakayotolewa na maofisa wa klabu ya Sevilla kwa viongozi wa klabu, TFF na washirika wake ili wapate kuimarika kitaaluma na kupata uelewa jinsi ya kuongeza mapato,”amesema Tarimba.
Naye Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Salum Madadi amemtaja mwamuzi wa kati wa kimataifa wa Tanzania, Herry Sassi ndiye aliyeteuliwa kuchezesha mchezo huo atakayesaidiana na Mohamed Mkono (Tanga), Soud Lila (Dar) huku mwamuzi wa akiba akiwa ni Jonesia Rukyaa (Kagera).
“Waamuzi wanaochezesha mchezo huu wote ni waamuzi wenye beji ya Fifa, mchezo huu mbali ya kujitangaza kama nchi lakini pia ni sehemu ya kutangaza vitu vyetu mbalimbali wakkiwemo wachezaji na waamuzi wetu,”amesema Madadi.
Kwa upande wa Simba, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa timu hiyo, Haji Manara amesema kuwa “Bado tunaendelea kuwashukuru SportPersa kwa kufanikisha ujio wa Sevilla nchini, ni fursa ambayo kila timu ya soka Afrika ingetamani kuipata.
“Maandalizi ya mchezo huo na Sevilla yanaendelea vizuri, timu imeelekea Singida kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara tutakaocheza kesho huko Namfua na mara baada ya mchezo huo timu itarejea kwa ajili ya kujiandaa na pambano hilo,”amesema Manara.


ReplyForward
IMEWEKWA NA Dizo One @ 3:52 PM
Email ThisBlogThis!Share to XShare to Facebook
Labels: Kimataifa
Next
Newer Post
Previous
Older Post

0 COMMENTS:

Post a Comment

Subscribe to: Post Comments (Atom)

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV
B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic




JIUNGE NA SALEH JEMBE SPORTS INSTAGRAM, GONGA HAPA, UPDATES KAMA ZOTE

BONYEZA HAPA KUJIUNGA NASI INSTAGRAM! KWA UPDATES ZOTE ZA MICHEZO

JIUNGE NA MIMI HAPA

FACEBOOK

SPORTS GEAR & FOOTWEAR

SPORTS GEAR & FOOTWEAR

WADAU WA BLOG HII

ZILIZOSOMWA SANA

  • YANGA WAANZA MAZUNGUMZO NA YONDANI
      KELVIN Yondani beki mkongwe ndani ya Klabu ya Yanga ambaye aliachwa jumla baada ya mkataba wake kuisha inaeelezwa kuwa yupo kwenye mazungu...
  • SARPONG ACHEKELEA KUIBUKIA YANGA, ATOA AHADI HII
    MICHAEL Sarpong mchezaji mpya wa Klabu ya Yanga amesema kuwa anafurahi kujiunga na Yanga na anaamini kwamba atapambana kufikia malengo ya ti...
  • MAJUKUMU MAPYA YA SENZO WA SIMBA NDANI YA YANGA HAYA HAPA
      KLABU ya Yanga leo Agosti 24 imemtambulisha rasmi aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa kuwa mshauri wao. Senzo atashirikiana ...
  • SIMBA: YANGA ITAKUTANA NA BALAA LA BWALYA
      UONGOZI wa Simba umesema kuwa mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga ambayo inatarajiwa kupigwa Oktoba 18, Uwanja wa Mkapa im...
  • MASHABIKI YANGA WAOMBWA KUSAJILI WACHEZAJI WAWILI WA KIMATAIFA
      UONGOZI wa Yanga umesema kuwa una wachezaji wawili wazuri wa kimataifa ambao tayari umeshazungumza nao ila unapenda kurejesha usajili wao ...
  • SAKATA LA MORRISON LAIBUKA TENA, YANGA KUIPOKA SIMBA UBINGWA
      K AMA ulikuwa  unadhani Klabu  ya Yanga  inatania katika  kesi yao dhidi  ya Bernard Morrison  basi jua kuwa klabu hiyo  ipo siriazi na hi...
  • FT: SIMBA 0-1 RUVU SHOOTING
      FT:Simba 0-1 Ruvu Shooting  Dakika 90 zinakamilika Mabingwa watetezi Simba wanayeyusha pointi tatu mbele ya wanajeshi Ruvu Shooting kwa ku...
  • ZAHERA: TUMEIBIWA POINTI 10 LIGI KUU
    Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amelalamika kuwa wameibiwa pointi 10 katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Kocha huyo amefunguka kwa k...
  • WIKI YA WANANCHI YAPAMBA MOTO, TIMU YA BURUNDI NDANI YA BONGO
      KLABU ya Yanga, imeanza sherehe zao kuelekea kilele cha Wiki ya Mwananchi ambapo uzinduzi ulifanyika rasmi jijini Dodoma Agosti 22 na kuhu...
  • SENZO WA SIMBA APEWA MASUALA YA LA LIGA YANGA
    UONGOZI wa Yanga umesema kuwa utafanya kazi kwa ushirikiano na aliyekuwa Mtendaji Mkuu ndani ya Klabu ya Simba, Senzo Mbatha kwa kuwa ni mtu...
index.jpg
 
COPYRIGHT © SALEH JEMBE HAKI ZOTE ZIMEHIFADHIWA
BLOG DESIGNED BY SALEH JEMBE =>TANZANIA SPORTS
•