May 13, 2019



KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa amewaambia wachezaji wake anataka pointi tisa za haraka ili kupata ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Akizungumza na Saleh Jembe, Aussems amesema kuwa kwa sasa amekuwa na wakati mgumu wa kupata matokeo kutokana na wachezaji wake kuchoka ila amewapa kazi moja kumtafutia pointi tisa ili kubeba ubingwa.

"Najua kwa sasa wachezaji wangu wamechoka kutokana na kucheza michezo 10 ndani ya siku 24 ila hilo nimewaambia waliache kwanza watafute pointi tisa ili tutwae ubingwa.

"Uwezo wao umepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na uchovu ndio maana nimekuwa nikibadilisha kikosi changu, ninaamini katika michezo sita iliyobaki tunapata pointi tisa, tena hata kabla ya kumaliza mechi zote, hili linawezekana," amesema Aussems.

Kama Simba leo itashinda mbele ya Azam FC itabakiza pointi sita ili kutangazwa kuwa bingwa msimu huu akimenyana na Yanga ambayo ipo nafasi ya pili na ina pointi 80.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic