May 13, 2019


WINGA wa kikosi cha KMC, ambaye alitikisa nyavu za mlinda mlango wa Simba, na timu ya Taifa Aishi Manula  kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara uliochezwa uwanja wa CCM Kirumba kwa kuipa timu yake bao la kufutia machozi walipofungwa mabao 2-1, Hassan Kabunda amewaita viongozi wa Yanga mezani ili kujadili suala la mkataba.

Kabunda ni injini ndani ya KMC ambayo ipo nafasi ya sita baada ya kucheza michezo 35 imejikusanyia pointi 46 ambapo katika mabao 35 iliyofunga amehusika katika mabao 14 amefunga manne na ametoa pasi za mabao 10.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kabunda amesema kuwa amekuwa akitafutwa na watu wengi ambao wanahitaji kupata saini yake ikiwa ni pamoja na viongozi wa Yanga hivyo ameamua kuwaita mezani kujadili suala hilo.

"Nimekuwa nikiskia taarifa kuhusiana na kutakiwa kwangu na Yanga hilo mimi sina mashaka nalo kwa kuwa najiamini kwa uwezo nilionao, pia hakuna ambaye ananiogopesha kwenye soka letu naujua mpira na ndiyo kazi yangu hivyo kama wapo siriazi kweli wanapaswa wafuate utaratibu ili kupata saini yangu, kwani kwa sasa mimi ni mali ya KMC," amesema Kabunda ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu.

Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera ameliambia Championi Jumatatu kuwa suala la usajili msimu huu atalisimamia kwa ukaribu na ana imani atawapata wachezaji makini ambao amewaona wanafaa kwa ajili ya msimu ujao na Yanga wenyewe watapenda.  

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic