May 15, 2019

NAHODHA wa Simba, John Bocco amesema kuwa wataonyesha uwezo mkubwa mbele ya Sevilla kwenye mchezo wa kirafiki utakaochezwa uwanja wa Taifa Mei 23.

Sevilla ambao ni mabingwa mara tano wa UEFA watacheza na Simba ambao ni washindi wa nafasi ya tatu kwenye michuano ya SportPesa Cup.

"Tunajua utakuwa ni mchezo mgumu na wenye ushindani ila tupo tayari kuona kwamba tunapata matokeo chanya kwenye mchezo huo, hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi.

"Tunawashukuru SportPesa kutuandalia mchezo mkubwa na muhimu kwetu, ni nafasi ya kujitangaza kimataifa hasa kupitia timu kubwa," amesema Bocco.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic