May 17, 2019

KUNDI La muziki wa Injili, Zabron Singers lenye ngome yake wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, limewashukuru mashabiki wake kwa kuwapa sapoti na kukubali kazi zao hivyo kwa sasa wapo kwenye mpango wa kutoa albamu nyingine ya nne.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kiongozi wa kundi hilo, Japhet Zabron ambalo wengi wamewatambua kupitia wimbo wa Mkono wa Bwana amesema kweli wameuona mkono wa Bwana.

"Albamu yetu ya Tumeuona Mkono wa Bwana ni ya pili kwani tulianza na albamu ya kwanza ambayo inaitwa nawakumbuka, kwa sasa tunamshukuru Mungu tumepokelewa vizuri na bado tunaendelea kufanya kazi kwa ajili ya mkono wa Bwana," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic