BILIONI 1.5 KUWASHUSHA HAWA YANGA, YUPO WA FC LUPOPO
UONGOZI wa Yanga umepanga kumkabidhi Kocha Mkuu wa timu hiyo Mkongomani, Mwinyi Zahera kitita cha Shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya usajili msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
Fedha hizo atakabidhiwa kocha huyo Mei 18, mwaka huu kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambako kutakuwa na hafl a ya kuichangia timu hiyo. Kamati hiyo iliyokuwa chini ya mwenyekiti wake Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde ambayo imeahidi kukabidhi fedha hizo.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano, uongozi hu mpya wa Yanga chini ya mwenyekiti wake msomi, Mshindo Msolla umepanga kukutana na kocha huyo mara baada ya mchezo wa jana dhidi ya Ruvu Shooting uliopigwa Uwanja wa Uhuru, Dar.
Katika kikao hicho, uongozi umepanga kupokea bajeti nzima ya usajili ya msimu mpya itakayowahusisha wachezaji wapya na wale wa zamani ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu huu.
Kitita hicho cha bilioni 1.5 kinatosha kabisa kufanya usajili bab kubwa kwa kuanzia na mshambuliaji wa Gor Mahia, Jacques Tuyisenge na beki wa kati wa AS Vita, Litombo Bangala wao wanataka dola 200,000 kila mmoja (zaidi ya Sh Mil. 460 kwa kila mmoja), Farouk Shikhalo ambaye kipa wa Bandari ya nchini Kenya yeye anataka Sh Mil. 80.
Kiungo mkabaji, Duke Abuya na kiungo mshambuliaji, Harrison Mwenda wote wanaoichezea Kariobang wanataka dola 25, 000 (zaidi ya Shilingi Milioni 50 kwa kila mmoja), Rodrick Mutuma anayecheza nafasi ya ushambuliaji anayeichezea Lupopo FC ya Congo yeye dau lake ni 40, 000 (zaidi ya Shilingi Milioni 90).
Wengine wapya ni wazawa ambao ni viungo washambuliaji, Hassan Kabunda, Charles Ilanfya wote wanaoichezea KMC, Kenny Ally (Singida United) na Ayoub Lyanga kila mmoja amewekewa dau la Shilingi 30 milioni.
Wanaotarajiwa kuongezewa mikataba ni Mkongomani, Papy Tshishimbi ambaye yeye msimu huu ametengewa Shilingi milioni 80 wengine ni Gadiel Michael, Mrisho Ngassa, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ ambao hao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu nao wamekewa dau la Shilingi Milioni 30 kila mmoja.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano, Zahera amependekeza katika usajili wake wa wachezaji wazawa, dau la kila mmoja lisizidi Shilingi Milioni 30 ili kupunguza gharama za matumizi.
Kwa hiyo kutokana na hali hiyo, usajili wa wachezaji wote hao wasipopunguza madau yao ya usajili Yanga italazimika kutumia Sh bilioni 1.6 ikiwa ni ongezeko la Sh milioni 100.
“Kocha tayari amependekeza katika usajili wa wachezaji bajeti yao ni Shilingi Milioni 30 kwa wazawa pekee, kwani viwango vyao havitofautiani hivyo ni lazima wasajiliwe kwa dau hilo,”alisema mtoa taarifa huyo.
Kwa upande wa uongozi wa Yanga, Mwenyekiti Mkuu wa timu hiyo, Mshindo Msolla alisema: “Uongozi wetu umejipanga kusajili mchezaji yeyote atakayemuhitaji katika msimu ujao awe nje au ndani ya nchi, kikubwa tunataka kurejesha Yanga anga za kimataifa.
CHANZO: CHAMPIONI
MTAMKABIDHI VIPI ZAHERA TAREHE 18 MEI WAKATI MWENYEWE ZAHERA AMEAGA NA KUSEMA ATAREJEA NCHINI TAREHE 19 MEI ?
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteMimi nilifikiri kuwa Uongozi Mpya umeingia mambo yanaenda kuwa na "afueni" pale Yanga imekuwa tofauti....kwani wachezaji tegemeo wanauzwa....mechi za kuwania ubingwa wa ligi zikiendelea, sherehe za Michango zinasitishwa na kuahirishwa, Kocha anakimbia/kwenda nje kuuza mchezaji, ahadi hewa na michakato na uongo kila kukicha....sasa sijui wana nia ipi? Wanayanga hebu jibuni haya maswali kabla chombo "akijaenda mrama"....msipumbazwe, Simba wanafurahia hii hali yenu.....kumekuwa na jitihada za kuwapotosha na kuwahadaa na kuwaridhisha wakati chombo hakiendi sawa.....msilale Yanga amkeni....."wanawapetipeti" kwa lugha za kuwalainisha mitandaoni....lakini ukweli ni kuwa hawana nia ya kuona Yanga inaimarika.....Fanyeni uchunguzi kwani kila maoni ya kupata wachezaji bora, benchi bora la ufundi na mambo mengine ya kuimarisha timu yanapotolewa utaona wanasema msajilini mchezaji fulani (wa bei ya chini kutoka hapa Tanzania tena mwenye kiwango cha kawaida, na ambae anatoka Simba au hata timu nyingine hali kiwango chake hata Simba hafai) ....Yanga kama mnataka maendeleo msikubali kuyumbishwa takeni na himizeni yaliyo juu hasa nikimaanisha usajili wa wachezaji level juu). Pili suala la kubadilisha mfumo wa uendeshaji lazima wawekezaji waanze kutafutwa ndani ya miezi 3....
DeleteKuna upotoshwaji na nia ya kutaka kuwatoa Yanga "nje ya reli/mstari"....wanachama na mashabiki amkeni sasa hivi mkihoji hivi vitu kabla vitu havijaharibika.....Uongozi huu lazima hukidhi matakwa ya wanayanga kuwa na timu bora....lakini dalili ya mvua ni mawingu.....nina maana kila mtu alifikiri Yanga itafanya usajili bora na kuanza kusuka kikosi bora haraka, lakini hali si hivyo....wanauza wachezaji tegemeo (makambo, nasikia tetesi fei toto yuko njiani pia) bila kureplace hii si dalili nzuri
Mwisho wa Maoni...
Ukiona kocha anaondoka na mchezaji halafu mara paaap mchezaji kasaini timu nyingine?KAMUUZA...Mmesalitiwa.Si ni yeye aliyekuja nae pia Yanga.
ReplyDeleteNauza shati nikanunuwe mkate
ReplyDeleteKila wimbo utaimbwa na kila ubeti utaitikiwa na ni sawa na kumpigia mbuzi zeze.Issue sio kuchangishana pesa na ili kusajili wachezaji bali muhimu hapa kunahitajika mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu na bila kufanya hivyo ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.Pesa zinachangwa ili ununue wachezaji wa maana na kwa bei mbaya kama viongozi wanavyojisifu kuwa watanunua mchezaji yoyote na kwa gharama yoyote lkn sijui mishahara ya hawo wachezaji wataendelea kuchangishana? wanasema wanataka kikosi kipana kama cha Simba au Azam lkn wanajua monthly budget ya Simba/Azam wanawalipaje wachezaji wao?kwa kuendelea kutegemea kuchangishana kweli hata kama tunadai ni timu ya wananchi?hivi kuchangishana kufikisha bilioni moja mnaona ni rahisi kihivyo?Kwa zama hizi kweli kuna mtu or organisation yoyote yuko tayari kuzimwaga pesa zake kwenye michango na harembee kama za arusi? chonde chonde viongozi wapya jihadharini na plani za zima moto.
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
DeleteLakini walisema kuchangishana ni mpango wa muda mfupi mpaka wa kati rejea hadidu za Kamati ya Hamasa na malengo ya Uongozi mpya...mabadiliko ya kuwa na mwekezaji na kuiendesha timu kwa mapato yanayotokana na wadhamini, vyanzo vya mauzo, matangazo ya biashara nk...na kupata wawekezaji ndivyo vinalipa mishahara....mbona hilo liko clear!
DeleteUsajiri mzuri hakika
ReplyDeletetatizo letu wabongo tunapenda kutafuniwa bila kushiriki garama za mafanikio ktk maendeleo ya klabu zao mpira ni pesa na pesa inatafutwa kwa akili ndugu acha kukariri hii ni timu ya wanachii ,wewe unajiita yanga alafu ata kadi ya uwanachama ulipi ada yako ya 1000 au hata kadi huna alafu unataka yanga ipige hatua bila wewe kushiriki, yanga ikifanikiwa kuwahamasisha wanachama wake kufikia milioni mbili tu wawe wanalipa tu 1000 kwa ajili ya ada ya kila mwezi tunauwezo wa kutengeneza 2b kwa mwezi nahili jambo linawezekana sio msubiri mpaka mwekezaji aje awakute maskini hohehae ndio ana walalia na kukupeleka anavyo taka
ReplyDeleteHili lilishajaribiwa huko nyuma kwa klabu zote mbili (Simba na Yanga) lakini bado halijatosheleza mahitaji ya uendeshaji wa klabu hizi....ndio maana ya kutaka mabadiliko ili kukaribisha pato lingine kufidia palipokwama...linawezekana ulaya au America na Asia kwenye uchumi uliokomaa sio huu wa nchi masikini lazima utahitaji uwekezaji ili uendane na soka la kisasa
DeleteUsijidanganye kuwa klabu ya Yanga ina wanachama zaidi ya million 1 ...lete data na sio kuleta hadithi za kufikirika.Uchaguzi uliokuwa muhimu ulihudhuriwa na wanachama hai ambao hawakufikia idadi ya 2,000.Sasa hawo wanachama 2 million wa kufikirika watapatikana kwa kuhamasishana?acheni masihara.
DeleteYaani itakuwa n miujiza uongozi haujatimia hata mwezi mnaanza kupiga kelele ama kweli wapenzi wa Bongo ni vichwa ngumu.
ReplyDelete