May 24, 2019


YANGA kwa sasa ipo kwenye mpango wa kuboresha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao ambapo lengo lao la kwanza ni kuboresha mikataba ya wachezaji ambao wamependekezwa na kocha wa Yanga Mwinyi Zahera.

Zahera amesema kuwa, Mei 28 itajulikana mbivu na mbichi kwa wachezaji wake wote ndani ya Yanga ambao watabaki na wale ambao atawapa mkono wa kwa heri.

 "Tupo vizuri wala hakuna matatizo, wachezaji wote ambao tunahitaji kuwaongezea mkataba tumeshamalizana nao hivyo ni suala la muda tu, mei 28 namaliza ligi, hivyo muda huo utakuwa mzuri wa kuwatangaza wale nitakaokuwa nao ndani ya kikosi," amesema Zahera.

Orodha ya wachezaji 18 ambao msimu unapokatika na wao mikataba yao inafika ukingoni imeelezwa ni hawa hapa:-

Ramadhan Kabwili, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Pato Ngonyani, Gadiel Michael, Abdallah Shaibu, Said Juma na Matheo Anthony.

Mrisho Ngassa, Thaban Kamusoko, Papy Tshishimbi, Raphael Daud, Pius Buswita, Juma Mahadhi, Baruan Akilimali, Amissi Tambwe, Haruna Moshi na Ibrahimu Ajibu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic