May 12, 2019


Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera ameendelea kuwataja wachezaji Meddie Kagere na John Bocco ndiyo kivutio kwake.

Hii si mara ya kwanza kwa Zahera ikumbukwe hata hapo awali aliwahi kuwataja sambamba na James Kotei pamoja na Jonas Mkude.

Kocha huyo amefunguka kuwa anakongwa nyoyo na wachezaji hao kwa namna wanavyojituma kunako Ligi Kuu Bara.

Ameeleza kuwa wanajua kufanya kazi yao vizuri uwanjani kwa kupigania nafasi zao na ndiyo maana wamekuwa na msaada mzuri ndani ya timu.

Bocco na Kagere mpaka sasa wamekuwa na mchango mkubwa ndani ya Simba ambayo imeshafunga jumla ya mabao 69 huku ikiruhusu nyavu zake mara 14 peke.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic