June 15, 2019


Kuna uwezekano mkubwa aliyekuwa mchezaji wa Yanga kwa msimu uliomalizika hivi karibuni, Ibrahim Ajibu akatangazwa kusajiliwa na Simba.

Taarifa zinasema kuwa Ajibu tayari ameshamalizana na Simba kwa kusaini mkataba wa miaka miwili na atakuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo msimu ujao.

Jana Simba walimtangaza Beno Kakolanya ambaye aliachwa na Yanga kufuatia amdai ya fedha zake za mishahara na zile za usajili.

Endapo Ajibu atatangazwa atakuwa anarejea rasmi katika klabu yake ya zamani ambayo ilimlea tangu akiwa katika kikosi cha vijana.


3 COMMENTS:

  1. Inaonesha juhudi kubwa Sana kumshawishi mchezaji huyo asirejee Kule alipolelewa na kukuzwa pamoja na juhudi za kumraka abaki hapo alipo, kumkazania ende Mazembe na mwisho kumwendea mzazi wake zote hazikufuwa dafu. Huyo kijana la Kwanza anatazama maslaha take na Pia kachina mwenendo WA kususia mara Kwa mara

    ReplyDelete
  2. huyo ni mmoja kati ya wachezaji wengi wa kitanzania ambao hawajitambui.......unaachaje kwenda Mazembe eti kwa sababu ya Simba na Yanga?.Hata kama maslahi ya simba na yanga yangekuwa juu kuliko mazembe bado alistahili kuchagua kwenda mazembe.Samata alikubali kuacha Mshahara mkubwa na marupurupu ya mazembe akaenda Genk kwa mshahara mdogo kwakuwa alikuwa na malengo.Leo anaogelea kwenye dimbwi la mafanikio kutokana na kuangalia faida na malengo ya baadae na si sasa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Brother.....Wachezaji wa Kitanzania hawalitambui hilo,wanachoangalia ni hela za mfukoni wanazopata kutoka kwa wafadhili wakanunue mboga na zaidi labda kudanganywa na magari ya mtumba ya Sh.Million sita,hawaangalii mbali hata kidogo na ndio maana wengi wanashindwa kwenda nje kucheza soka la kulipwa kwa sababu kule hakuna cha kuamka na kwenda kwa mfadhili kumpiga mzinga mwisho wa siku mpira unapoisha wanabaki kusumbua watu mitaani kwa kuwapiga mizinga

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic