June 15, 2019


Baada ya aliyekuwa kipa wa Yanga, Beno Kakolanya kumwaga wino wa miaka miwili jana na wekundu wa Msimbazi, Simba SC, imeelezwa kuna wengine tayari wameshamalizana na miamaba hao wa Ligi Kuu Bara.

Taarifa zinasema tayari kuna wachezaji watano ambao tayari wameshamwaga wino lakini picha zao hazijaachiwa mitandaoni.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani kutoka Simba zinasema kuwa wachezaji hao ni Ibrahim Ajibu, Serge Wawa pamoja na Shomari Kapombe.

Mbali na watatu hao, wengine wanaotajwa kumwaga wino ni Mohammed Hussein 'Tshabalala' pamoja na Walter Bwalya ambaye anakipiga katika klabu ya Nkana Red Devils ya Zambia.

5 COMMENTS:

  1. Na vipi Yule WA Kenya aliyekuwa pacha na Kagere. Mambo inaonesha murwa kimyume aliyokuwa akiyatamani ndugu Ten

    ReplyDelete
  2. Nataka kusikia beki wa kati amesajiliwa.. Wawa ana homa na mechi za kimataifa akiwa ugenini. Huwa kama anapagawaga na mechi hizo. tutafutieni beki nguli kwa michuano ya kimataifa. mambo ya kupigwa tano msipoangalia yatajirudia tena.

    ReplyDelete
  3. Kweli huyu wawa bado kabisa mechi za ugenn anashindwa kujipanga simba inatakiwa itafute mtu wa maana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic