June 3, 2019



Kesi inayowakabili waliokuwa viongozi wa  Simba imeshindwa kuendelea kusikilizwa baada ya shahidi aliyeandaliwa  kufiwa na kushindwa kufika mahakamani.

Kesi hiyo inawakabili  hao waliokuwa viongozi wa Simba Evans Aveva na Godfrey Nyange 'Kaburu'  ambao wanakabiliwa na shitaka la kughushi na kutakatisha  fedha huku Zachariah Hans Pope akiunganishwa katika kesi hiyo yeye kwa kudaiwa kuwasilisha nyaraka za uongo za ununuzi wa nyasi bandia.

Kesi hiyo ilitarajiwa kuendelea leo Jumatatu kwa kusikilizwa ushahidi wa shahidi wa tano.

Wakili wa Serikali, Leonard Swai aliiambia mahakama kuwa tayari alikuwa ameandaa shahidi lakini alimpigia simu kuwa amefiwa mkewe hivyo ameshindwa kufika.

Hivyo Swai aliiomba mahakama kupangiwa tarehe nyingine kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa kesi hiyo.

Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Thomas Simba alisema upande wa serikali uhakikishe kuwa unaanda mashihidi  watatu ili akikosekana mmoja awekwe mwingine.

Swai ametakiwa kuleta mashahidi wengi watatu katika kesi hiyo ambayo inatarajiwa kuendelea  Juni 12 na 13 mwaka huu.

1 COMMENTS:

  1. tusiwasimange yanga na kibakuli chao tuwe tunaenda kuwatembelea hawa watu jela, nahisi bila wao kufanya walivyofanya japo tumezoea kulaumu yawezekana aibu yetu ingekuwa kubwa kuliko bakuli la yanga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic