MAHAKAMA imeshindwa kuendelea kusikiliza kesi inayowakabili waliokuwa viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya Serikali kushindwa kuleta shahidi.
Kesi hiyo ilitarajiwa kuendelea leo Jumatatu ambapo shahidi wa 14 angetoa ushahidi wake kwenye kesi hiyo.
Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai aliiambia mahakama kuwa hakupata muda wa kuandaa mashahidi kwa kuwa alikuwa amesafiri hivyo apangiwe tarehe nyingine.
Hata hivyo wakili upande wa washitakiwa, Richard Rweyongeza aliiambia mahakama upande wa Serikali wanatakiwa kutambua kuwa wateja wao wapo ndani hivyo ni vizuri kujipanga walau hata kuwa na mashahidi wawili ili kesi iweze kwenda.
Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Maira Kasonde alisema kuwa kesi hiyo imehairishwa mpaka Juni,10 mwaka huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment