June 4, 2019


MSEMAJI wa klabu ya Simba ambao ni mabingwa wa soka Tanzania Bara, Haji Manara, amesema ilibaki kidogo tu mwaka huu aachane na kazi hiyo kutokana na kile alichokisema ni changamoto nyingi za kiutendaji.

Manara amesema hayo leo Juni 3, katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, alipoongozana na wachezaji wa timu hityo walioshinda Tuzo za Mo Simba 2019,  zilizofanyika wiki iliyopita ambapo Makonda aliwaahidi kuwapatia pesa kama pongezi kwa kazi kubwa waliyofanya.

Katika hafla hiyo amepewa Sh. milioni tatu ambapo amesema milioni moja ataipeleka kwenye Kamati ya Sekretarieti ya Simba kutokana na kazi kubwa wanayofanya akishirikiana nao,  na laki tano atawapa Chama cha Walemavu ili iwasaidie katika mambo mbalimbali yakiwemo ya michezo.

Aidha, amemshukuru Makonda kwa zawadi hiyo na kuwataka wananchi na vyombo vya habari kumuunga mkono kwani anachokifanya ni kwa maendeleo ya taifa kwa jumla.

Katika ahadi yake Makonda aliahidi kuwapa milioni moja  kila mchezaji, isipokuwa Manula aliyepata milioni 10 na mchezaji bora wa kike wa klabu hiyo, Mwanahamisi milioni mbili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic