June 4, 2019


Kiungo mshambuliaji mkongwe wa Yanga, Mrisho ngassa amesema kuwa ana ofa nyingi hivi sasa kutoka timu za hapa nchini na nje ya nchi ikiwemo Zambia na kama mipango ikikaa sawa basi ataondoka Jangwani.

Licha ya kuwepo kwa ofa hiyo, Ngassa amesema tayari ameshapata taarifa kutoka kwa mabosi wake wakimuomba kuongea naye kwa ajili ya kuongea mkataba.

Ameeleza kuwa amepewa taarifa hiyo na endapo mazungumzo hayatafanikiwa basi ataangalia sehemu nyingine kwa ajili ya kwenda kucheza ikiwemo Zambia.

“Nimepata taarifa kutoka uongozi juu ya kuniongezea mkataba mpya wa kubaki Yanga, lakini bado hatujakaa rasmi mezani kujadili mkataba huo.

"Hivyo nawasubiria mabosi hao na kama tukishindwana basi nitaangalia sehemu nyingine ikiwemo kwenda Zambia.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic