June 4, 2019


Imeelezwa kuwa beki wa klabu ya Yanga, Abdallah Shabibu 'Ninja' amefunguka kwa kueleza kuwa yupo tayari kujiunga na mahasimu wao wa jadi Simba endapo watakubaliana.

Ninja amesema tayari ameshamaliza mkataba na Yanga ambapo kwa msimu ujao anaweza akawa na timu yoyote ile endapo hawatakubaliana kuongeza mkataba mwingine.

Taarifa imeeleza kuwa beki huyo aliyekuwa moja ya wachezaji tegemo Yanga kwa msimu uliomalizika siku kadhaa zilizopita, ameeleza yupo tayari kujiunga na timu yoyote hata Simba kama wakihitaji huduma yake.

Ninja amesema tayari wameshaanza mazungumzo na Yanga kwa ajili ya mkataba mpya ingawa ameweka tahadhari kama wakishindwana basi atakuwa tayari kutua popote.

Mpaka sasa hajajulikana juu ya hatma mchezaji huyo kama ataendelea kusalia ndani ya mabingwa hao wa kihistoria kutokana na ingizo la wachezaji wapya ambao unaendelea kufanyika mpaka sasa.


2 COMMENTS:

  1. Hahaha. Mabingwa WA kihistoria muandishi inampa Raha sana

    ReplyDelete
  2. Simba wanatakiwa kumsaini Abdallah kwani kiufundi Shaibu ni beki namba sita ngangari anahitaji marekebisho madogo tu na Simba hawata juta kumsaini.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic