June 15, 2019


KUELEKEA kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2019/20 Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa, na Michezo, Dr.Harrison Mwakyembe amesema kuwa wachezaji wa kigeni watakaopata nafasi ya kucheza hawatazidi watano.

Sheria hii haitaangalia ukubwa wa timu iwe Yanga ama Simba, Lipuli, Azam FC na nyingine zote lazima zifuate.

Mwakyembe ameyasema hayo leo kwenye hotuba ya
ke ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo kulikuwa na Tamasha la Kubwa Kuliko maalumu kwa ajili ya kuichangia timu ya Yanga kupata fedha za kujiendesha.

"Msimu ujao nataka kuona sheria zinabadilika hasa kwa wachezaji wa kigeni ambao watacheza ligi, ukisajili wachezaji 100 wa kigeni hatuna tatizo ila watakaocheza uwanjani hawatazidi watano ama wanne, na hili ninalisimamia kwa ukaribu.

"Sheria zipo na hazifuatwi hivyo hakutakuwa na ruhusa kwa timu ambayo haina timu ya vijana kushiriki Ligi Kuu Bara, tunataka tujenge timu bora ya Taifa hivyo lazima uwekezaji uwe mkubwa," amesema Mwakyembe.

6 COMMENTS:

  1. Nafikiri ni hoja dhaifu sana....huwezi kuimarisha viwango vya wachezaji wazawa au ligi yetu kwa kuzuia ushindani toka kwa professionals.England, spain, france etc wangefanya hivyo ingekuweje?.Safar hii tumefanikiwa kwenda afcon kwasababu angalau wachezaji wanaocheza ligi ya ndani wameiva kwa kupata ushindani kutoka kwa wachezaji wa kigeni.

    ReplyDelete
  2. duh huku ni kuturudisha nyuma.Kanuni za soka hazitungwi na serikali na mwenye ligi ni TFF.Nitawashangaa serikali ikiingilia TFF.kwanza timu za majeshi na polisi kisheria hawatakiwi kuwa mwanachama wa TFF.

    ReplyDelete
  3. Mbona haya hayakutokea wakati Simba waliporundika rundo la wachezaji wa kigeni na kanuni kubadilishwa ili wapate nafasi ya kucheza? iweje leo baada ya kuona Yanga wanajizatiti na usajili wa wachezaji wa kimataifa ndo waziri aje na tamko hili? Ametumwa au????

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tumia busara kufikiria kwani hao Simba hawataumia na hizo sheria??

      Delete
  4. Kitu wanachopaswa serikali kuelewa ni kuwa soka kwa sasa ni biashara na sio ridhaa.Muwekezaji huwezi kumwekea masharti ya kufanya biashara ambao anajua wazi hailipi.Timu yetu ya Taifa imeanza Afcon baada ya kusotea zaidi ya miaka 30 na wachezaji wengi wa kigeni wakicheza kwenye ligi yetu na sijui wameathiri kitu gani.Maamuzi Kama haya yahitaji mtu mmoja kuamrisha kuwa mwaka huu nataka ligi iwe hivi.Viongozi wote wa vilabu wanakutana na kujadiliana ligi iendeshwe kwa mtindo gani.Mimi nalipinga hili la waziri kusema 5 players wageni ndio watakaocheza kwani halina mantiki na hii ni Kama kuwalea wazawa kutojitambua... Ushindani kwa wazawa ni pale watakapogombania namba na wageni. Vinginevyo ni kutwanga maji kwenye kinu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic