June 24, 2019


BAADA ya hivi karibuni mshambuliaji wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi kudaiwa kugoma kuongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia timu hiyo, sasa mambo yamekaa sawa.

Habari njema kwa mashabiki wa Simba ni kwamba Okwi ambaye sasa yupo na kikosi cha timu ya taifa ya Uganda michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2019) anadaiwa kukubali kuongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia Simba.

Inadaiwa Okwi anaelekea kufikia hatua hiyo baada ya kufanya mazungumzo na mmoja wa viongozi wa Simba huko nchini Misri ambaye pia aliambatana na baadhi ya Wabongo ambao ni wapenzi na mashabiki wakubwa wa timu hiyo.

Akiwa na kikosi cha Uganda, juzi Jumamosi, Okwi alikuwa Mchezaji Bora wa Mechi dhidi ya DR Congo baada ya kufunga bao moja katika ushindi wa mabao 2-0.

“Okwi anaelekea kukubali kuongeza mkataba mwingine wa kuendelea kuitumikia timu yetu baada ya kufanya mazungumzo hivi karibuni na uongozi lakini pia baadhi ya wabunge ambao ni wapenzi na mashabiki wa timu yetu.

“Mazungumzo hayo yamefanyika huko nchini Misri ambako yupo na timu ya taifa ya Uganda katika Afcon. “Kwa hiyo ni matumaini yetu kuwa kama hatobadili tena msimamo wake basi muda wowote atasaini mkataba wa kuendelea kuitumikia timu yetu,” kilisema chanzo hicho cha habari.

Alipotafutwa Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori hakupatikana kutokana na simu yake mkononi kuita tu bila ya kupokelewa kama ambavyo pia ilikuwa kwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Swedy Mkwabi.

Mbali na makubaliano hayo, inaelezwa kuwa mara baada ya kuondoka nchini, Okwi alibadili namba ya simu kwa kuwa namba aliyokuwa akiitumia awali haipatikani hadi sasa, hivyo ilikuwa ngumu kumpata kwa njia ya simu.

3 COMMENTS:

  1. Jambo la busara waharalishe fasta kabla ya mechi yao ya pili Uganda kwani kuna uwezekano mkubwa Okwii kuwa Lulu Misri kazi ya kumgombania Simba na timu nyengine itakuwa kubwa.

    ReplyDelete
  2. Ina maana kuna watanzania wamesafiri kwenda Misri kwa ajili ya Uganda?

    ReplyDelete
  3. Nilikuwa nikimuangalia kwa Undani zaidi Emanueli Okwii ndani ya kikosi cha timu ya Taifa Uganda zidi ya Congo.Halafu nikamungalia kwa Undani zaidi John Raphaael Boko ndani ya kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania zidi ya Senegal halafu nikajiuliza mimi mwenyewe peke yangu kama kweli Simba tulifanya uchaguzi na kuchagua viongozi makini kuhakikisha timu yetu haifanyi maamuzi ya hovyo ya kiutendaji?
    Simba walizembea mpaka dakika ya mwisho kumuongezea mktaba Okwii halafu kukawepo na tuhuma kuwa Okwii anawadengulia Simba?
    Kwa maoni na mtazamo wangu naona ni Simba ndio waliokuwa wakimdengulia Okwii na kumkosea heshima nadhani hata wakati mwengine Okwii kuonekana mchazaji wa kawaida ndani ya kikosi cha Simba ni Kutokana na kutokuwa na furaha na baadhi ya mambo yanavyokwenda ndani ya Simba zidi yake. Na muheshimu Boko lakini ilikwenda kwenda vipi mpaka John Boko akawa Capteni wa Simba na isiwe Okwii aliewafanyia mambo makubwa na ni miongoni mwa wachezaji wa Simba ambao wamedumu kwa kipindi kirefu na kuwatengenezea pesa pia nzuri tu. Vipi Simba wachukue maamuzi ya haraka ya kumsajili John Boko fasta ambae ameikosea heshima klabu na viongozi kwa kuingia kandarasi ya mkataba wa awali na timu ya Africa kusini bila ya kuujulisha uongozi lakini wakampuuzia Okwii mapaka hivi sasa bila ya kufanya jitihada za makusudi za kumshawishi mgamda huyo kuongeza mktaba? Okwii ni mchezaji mkubwa na yeye mwenyewe anajielewa hivyo na ananitambua na ni maamuzi yake mwenyewe binafsi kubakia kufanya kazi Africa ila hata ulaya angeenda angeliweza kuweka alama za kukumbukwa. Na nionavyo ni kana kwamba kuna kauzembe fulani ndani ya uongozi wa Simba kuhusiana na suala la Okwii. Licha Okwii kuja Tanzania kutoka Uganda lakini unaweza kusema kuwa Okwii ni moja ya kati ya zao la Simba la kujivunia na nadhani Simba wanapaswa kuwa makini zaidi na Okwii kama machezaji muandamizi wa klabu na sio kumchukulia kirahisi rahisi tu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic