June 4, 2019


LICHA ya uongozi wa Simba kumuita mezani beki wake Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ kwa ajili ya mazungumzo ya mkataba mpya meneja wa nyota huyo amefunguka kuwa wanaangalia na upepo wa Afcon unaenda vipi kutokana na ubora wa mchezaji wake.

Tshabalala ni mmoja kati ya wachezaji ambao mikataba yao imemalizika pamoja na Haruna Niyonzima, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Aishi Manula na Said Mohammed. Harry Chibakasa ambaye ni meneja wa beki huyo alisema;

“Uongozi wa Simba tayari umetuita mezani kwa ajili ya mazungumzo ya mkataba mpya hilo halina tatizo kwa sasa pia tunangaalia kule Afcon mambo yanakwendaje kwanza hivyo tutachelewa kidogo.”

“Sababu Tshabalala ni mchezaji mwenye mafanikio kwa sasa ambapo ametoa mchango mkubwa kwa timu yake kutwaa ubingwa mara mbili jambo ambalo sio dogo na linatakiwa kuangaliwa kwa umakini mkubwa kabisa,”alisisitiza.

9 COMMENTS:

  1. Shabalala ni mchezaji mwenye mafanikio lakini Simba ndio iliyompa mafanikio hayo.Hata hivyo nikimwangalia shabalala licha ya ubora wake lakini ana mapungufu kadhaa wa kadhaa na kama ningekuwa mimi ndie shabalala basi ningekuwa wa kwanza kuharakisha kusaini mkataba mpya pale Simba. Mohamedi Hussein anatakiwa kukomaa au kujikomaza zaidi kifitness na kiumakini zaidi ili afikie kiwango cha kuitetemesha Simba kunako usajili kwani ni rahisi tu Simba kutafuta beki tatu ambae anaweza kumpa shabalala wakati mgumu. Mfano Simba kama inavyosemekana kuwa wapo mbioni kumsaini Gadiel Maiko wa Yanga huyo kijana pekee itakuwa changamoto tosha kwa shabalala.

    ReplyDelete
  2. Kwa kiasi kukubwa sana, nakubaliana kabisa na yote uliyoyasema juu ya mchezaji huyu!! Tukumbuke pia Asante Kwasi alipokuwa fit alivyokuwa akimweka bench!

    ReplyDelete
  3. Nimekwisha ona hawa wachezaji wa Simba pengne hawana fadhila ila najua kila mtu anakimbilia AFCON najiuliza afcon tukitolewa makundi na ni mechi tatu na ukiangalia wengi watakaa bench au majeraha, watakiwa watazame mbali wakijua kuwa Afcon kuna lundo la wachezaji kwa kuchelewa kuna mambo mawili kuachwa au kunogeshwa mtu unajua mm naanzia benchi kundi tulilopo ni gumu bado unasema mpaka michuoni iishe haya na viongozi wa Simba wasimbembeleze mtu kisa kuchukua ubingwa ila waangalie atakae wafaa ni nan, Ukiangalia mtu kama manula, Nyoni, kagere, chama, wao watasemaje na kiukweli kazi imeonekana da lakin wabongo hapo ndo tumepata pa kupandia sasa, wengne wakipata mafanikio hawaondoki ili wayatunze yale mafanikio wengne ndo sasa wamefika mwisho wakumbuke Tanzania kuna wachezaji weng sana hasa mabeki wapo wengi mno ila hawaangaliwi. Chezeeni fursa sasa

    ReplyDelete
  4. Swadakta Nyamsana, uko sahihi kbsaaaa! Wachezaji wetu wanatakiwa wajielewe, na wajifanyie 'self-evaluation'!

    ReplyDelete
  5. sbabalala aliisababishia simba hasara ya magoli a ya uzembe wake wa kusndwa kukaba na kusindikza winga au kuruhusu winga kupiga cross kirahisi kwenye CAF Championship. Kumbuka goli la Nkana Dar ilikuwa ni makosa ya Tshabalala. Goli la Saoura kule Algeria alishindwa kuzuia krosi. Kumbuka goli la 4 la TP Mazembe aliruhusu krosi ya kizembe kupigwa na winga kijana wa miaka 20 tu tena kwa yeye shabalala kuburuzwa kirahisi. Kumbuka goli la 2 la AS VITA kule DRC ambapo alitoa pasi mbovu sana kwa Chama kisha ikanaswa na simba mpira ukaenda kuwa goli.

    ReplyDelete
  6. simba waachane nae wamchukue GADIEL Maiko na Walusimbi wa Uganda ambaye uwa haruhusu krosi za kijinga na ni mkomavu sana kwenye mechi kubwa na cha msingi zaidi yuko huru. Anacheza Cranes na yuko Abu Dhabi dakika hii

    ReplyDelete
  7. Mwacheni aringe gari itamuaccha

    ReplyDelete
  8. Viongozi achaneni nae...Mchukueni hata Paul Ngalema wa lipuli.Huyo kwenye hclub bingwa katugharimu sn.....angejua angenyamaza kimya asije akaibua hasira kwani tunamstahi tu.Ngalema+Walusimbi wanatosha

    ReplyDelete
  9. Ni mchezaji wa kawaida ashukuru nyoni alivyokuwa anaficha madhaifu yake hata kwenye afcon hawezi kupata namba wamwache aende

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic