IMEELEZWA kuwa baada ya Yanga kupata zali la kukwea pipa msimu ujao kwa sasa nguvu kubwa ni kwenye usajili ambapo tayari wameanza kuonyesha makeke yao huku wakiendelea kuwapa mikataba ya awali baadi ya wachezaji.
Pia imeelezwa kuwa kuna mkakati wa kuboresha benchi la ufundi ambapo wanamtazama kwa ukaribu Mecky Maxime Kocha Mkuu wa Kagera Sugar afanye kazi na kocha Mwinyi Zahera ambaye amesema bado hajakubali maamuzi hayo.
Hawa hapa wachezaji ambao wanatajwa kuwindwa na kikosi hicho cha mabingwa wa kihstoria Tanzania wakiwa wametwaa ubingwa mara 27.
Salum Aiyee mshambuliaji wa Mwadui FC.
Aaron Lulambo mlinda mlango wa Tanzania Prisons.
Ally Sonso beki wa timu ya Lipuli.
Francis Kahata, mshambuliaji wa Gor Mahia.
Hassan Kabunda winga wa KMC.
Salum Ilanfya, mshambuliaji wa KMC.
Ally Ally beki wa KMC.
Said Ndemla, kiungo wa kikosi cha Simba.
Jonas Mkude, kiungo wa timu ya Simba.
Ayoub Lyanga, mshambuliaji wa Coastal Union.
Hehehe 😋 mimi nacheka tuu,
ReplyDeleteMara wanasema hawana haja na wachezaji WA Simba na kumbe masikini Roho yao inawatamani. Vipi Ajibu hawamtaki. Mabingwa WA jadi vigeogeo sana
ReplyDeleteYanga wanaonekana nakuwa na kiherehere cha kuifuata fuata Simba kwenye nyao zake na sijui lengo nini. Na nadhani kama ingelikuwa ni Simba yenye kufanya hivyo basi sijui kelele za Yanga zingekuwa za kiasi gani. Mafanikio ya Simba yamekuja licha ya usajili mzuri walioufanya msimu uliopita lakini pia kumetokana na hamasa za mashabiki wake,uekezaji au Muekezaji Simbadamu ambae hulka yake kubwa zaidi ni kutaka kuona Simba anakuwa Simba wa ukweli sio maneno tu. Pia benchi la ufundi kamili na mpangilio bora wa safu ya uongozi wenye zamira ya kuiona Simba inakuwa bora. Huwezi kuizoofisha Simba kwa kutaka kusajili kila mchezaji wa Simba au kutaka kumsajili kila mchezaji anaetakiwa kusajiliwa na Simba. Si dhani kama Yanga wapo tayari kwa vita ya usajili zidi ya Simba licha ya kelele nyingi mitaani. Wachezaji hawa wanaowasajili Yanga hivi sasa sidhani kama ni aina ya wachezaji watakaokubali kuja kucheza bure kama walivyokuwa wakiwafanyia wachezaji wazawa licha ya ubabe wa Zahera. La kama Yanga wapo vizuri kiasi hicho yakwamba mishahara ya wachezaji wake itakuwa haina shida in time kama Simba au kuliko Simba basi sisi ndivyo tunavyoomba na itakuwa faraja kwa soka la Tanzania lakini isijekuwa kama singida united mbwembwe nyingi kocha wa kizungu halafu aibu tupu hata kula ya kocha shida achilia mbali mishahara.
ReplyDeleteHayo ni maneno ya mwandishi. Yanga ipo wazi sana, hakuna mchezaji wa simba atakaye sajiliwa na Yanga msimu huu. Hao wachezaji watasajiliwa na Salehe wakacheze ndondo.
ReplyDeleteMsimu wa usajili ndio kipindi Cha uzushi Ili watu wauze magazeti
ReplyDelete