MABINGWA watetezi Azam FC leo watakuwa kazini kumenyana na KCCA kwenye michuano ya Kagame inayoendelea nchini Rwanda.
Mchezo wa kwanza Azam FC walipata ushindi wa bao 1-0 mbele ya wapinzani wao Mukura FC bao lililopachikwa kimiani na Idd Seleman.
Kocha wa Azam FC, Ettiene Ndayiragije amesema kuwa wanatambua ugumu wa mashindano kutokana na kikosi chake kushindwa kuwa na spidi kali.
"Mashindano sio mepesi tatizo la kwenye mchezo wa kwanza ilikuwa ni spidi ila nimefanyia kazi na tutapambana kupatamatokeo chanya," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment