July 9, 2019

DEOGRATIUS Munish 'Dida' ambaye kwa sasa yupo huru baada ya kumaliza mkataba wake na Simba yupo kwenye hesabu za kuvutwa ndani ya kikosi cha Coastal Union ya Tanga.

Mlinda mlango huyo ambaye amewahi kuitumikia pia timu ya Yanga na Mtibwa Sugar zamani amesema kuwa bado hajajua ni timu gani ataitumikia msimu ujao ila habari zimedai kwamba huenda ataibukia Tanga.

Coastal Union iliyo chini ya kocha, Juma Mgunda kwa sasa ipo kwenye mazungumzo na Dida endapo mambo yatakaa sawa ataitumikia msimu ujao.

Mgunda amesema kuwa mipango ya usajili ipo ila ishu ya kutaja majina ya wachezaji kwa sasa ni ngumu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic