July 7, 2019

IMEELEZWA kuwa beki wa Yanga, Gadiel Michael amemalizana na Simba kwa kandarasi ya miaka miwili kwa ajili ya kukitumikia kikosi hicho msimu ujao.

Michael alipishana na Yanga kutokana na kumuwekea dau dogo jambo ambalo limemfanya aamue kujiunga na Simba ili kumfuata rafikiye wa karibu Ibrahim Ajibu.

Chanzo cha kuaminika kimeeleza kwamba tayari Gadiel amemalizana na Simba hivyo anachosubiri kwa sasa ni kutambulishwa.

"Tayari Gadiel amemalizana na Simba na amesaini kandarasi ya miaka miwili, amefanya hivyo baada ya kuwekewa dau kubwa tofauti na lile alilowekewa Yanga,"kilieleza chanzo hicho.

Gadiel Michael mwenyewe amesema kuwa hana tatizo kumwaga wino ndani ya Simba kwani yeye ni mchezaji hachagui kambi.

"Hakuna tatizo kwa mimi kusaini Simba kwani mchezaji hachagui kambi, hivyo kama Yanga nimeshindwana nao sioni taabu kusaini Simba, na itafahimika muda si mrefu kuwa nimesaini Simba," amesema Gadiel.

5 COMMENTS:

  1. Yeye atapambana na Yule aliyetoka Uganda

    ReplyDelete
  2. Hebu kuweni serious nyie Yanga mnaenda kushiriki CAF CL halafu mnasajili rookie? Hebu toeni mkopo Kindoki wekeni Walusimbi au Batambuze....msitutie aibu CAF mwisho tuzipoteze nafasi zetu 4 za CAF Competitions

    ReplyDelete
  3. Ila mwisho wako dogo utakuwa mbaya. Nahis akili yako ndogo. Azam ulitoka kwa maneno na leo umetoka Yanga kwa kujiona wewe star. Mpira hauko hivyo.
    Pole sana kijana

    ReplyDelete
  4. Bado Simba haijatatua tatizo la mabeki wa maana.....beki #3 anatakiwa mtu mwenye uwezo na Uzoefu wa CAF...hawa mabeki (Gadiel & Tshbalala) hawawezi kuzuia forward kali za Esperance, TP Mazembe, Raja Casablanca walioenda juu na wenye kushiba na wenye kasi....tofauti za uchezaji kwa Gadiel na Tshabalala hakuna... NARUDIA tena ni mara mia (100×) Simba tumsajili WALUSIMBI NAMBA 3 KULIKO GADIELI....TUNZA KUMBUKUMBU YA COMMENT HII MTAKUJA KUNIAMBIA.......Simba tunataka mabeki wazoefu na CAF CL....sio mabeki wa kuwazuia lipuli, Ndanda, na alliance!!....huko sie tumeshatoka.....tunadeal jinsi ya kushindana na Esperance, TP Mazembe, Raja Casablanca haswa mechi za ugenini....kwahiyo akina Gadieli hawatatusaidia kitu....hakuna tofauti na Tshabalala!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic