BENO
Kakolanya, mlinda mlango wa Simba ameanzishiwa program maalumu itakayomfanya
awe fiti msimu ujao akiwa nchini Afrika Kusini.
Kakolanya
amesajiliwa na Simba msimu huu akitokea Yanga kwa kandarasi ya miaka miwili ana
kazi ya kumuonyesha Kocha Patrick Aussems msimu ujao ili kupenya kikosi cha
kwanza kwa kumuweka benchi Aish Manula.
Kakolanya amesema kuwa ana furaha kuwa ndani ya kikosi
cha Simba ana imani kubwa ya kufanya vema msimu ujao.
“Huku
tunapambana kujiweka sawa na kila mchezaji anaendelea vizuri kwa kuwa sawa kwa
ajili ya msimu ujao na imani ni kubwa kwamba tutapambana.
“Suala la
namba kwa sasa sio kipaumbele changu kwa kuwa mimi sipangi kikosi hilo lipo mikononi
mwa mwalimu cha msingi ni mashabiki kuzidi kutuombea,” amesema Kakolanya.
Simba imerithi dume la kuaminika. Atawaliza watu huyu
ReplyDelete