July 29, 2019

ETTIENE Ndayiragije, Kaimu Kocha wa timu ya Tanzania 'Taifa Stars' amesema kuwa sare waliyoipata imetokana na kushindwa kutumia nafasi walizozipata hivyo ni muda wa kufanyia kazi makosa waliyoyafanya.

Stars jana ilikubali suluhu ya bila kufungana na timu ya Taifa ya Kenya kwenye mchezo wa kwanza wa kufuzu michuano ya Chan itakayofanyika Cameroon mwaka 2020.

"Wachezaji wamejituma na wamefanya kazi kwa juhudi, kilichoshindikana ni kutumia nafasi ambazo wamezipata hivyo ni wakati wetu kujipanga kwa ajili ya mchezo wa marudio nchini Kenya.

"Sapoti ya mashabiki ina nguvu nasi pia tunajipanga upya kwani kwenye mchezo yote ni matokeo licha ya kutokuwa na mpango wa kupata sare," amesema. 

Stars itamenyana na Kenya mchezo wa marudio kati ya Agsti 4 nchini Kenya.

1 COMMENTS:

  1. Capteni Boko kama kiongozi anatakiwa kujiamini na kuwa makini na mtuluvu zaidi anapoingia kwenye kumi na nane za adui. Halafu tatizo liko wapi? Au ndio maelekezo ya kocha? Kanini mafowadi na wachezaji wa viungo wanashindwa kupiga mashuti golini.Tuna wachezaji kama Hasani Dilunga na Sure boy hawa wote ni wapigaji wazuri wa mashuti inashangaza mpaka kipindi cha kwanza kinakwisha Taifa stars wakiwa nyumbani wamejaribu mashuti mawili basi golini? Kwa ujumla timu imecheza vizuri na kwakweli imeonesha kama hii timu ikitunzwa vyema na kumpa kocha na benchi lake la ufundi muda wa kutosha wa kukaa pamoja na wachezaji basi tutafanikiwa. Ila kwa game na wakenya umakini ulikosekana kwa fowadi line na kazi kubwa inatakiwa kufanywa katika eneo hilo kabla ya mechi ya marudiano.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic