UONGOZI wa
KMC ambayo ilikuwa inashiriki michuano ya Kagame nchini Rwanda umesema kuwa kwa
sasa nguvu zote ni kwenye maandalizi ya Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza
Agosti 23.
KMC kwenye michuano ya Kagame imekusanya pointi tatu baada ya kucheza michezo mitatu ambapo
ilipoteza mbele ya TP Mazembe kwa kufungwa bao 1-0 ilishinda mbele ya Rayon
Sports kwa bao 1-0 na kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Atlabara
kwenye kundi A.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa KMC, Anwar Binde amesema kuwa
ushindani ulikuwa mkubwa na wanaamini kuna kitu wamejifunza.
“Timu
ilikuwa inajenga muunganiko mpya hivyo wachezaji wamepambana kwa uwezo wao na
nimependa namna ambavyo wamefanya kitu kizuri.
"Kwa sasa timu itaweka kambi Dar na kama itatokea itakuwa nje ya hapo tutatoa taarifa mapema kikubwa sapoti na maandalizi ya ligi kwa msimu ujao," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment