July 4, 2019


Uongozi wa Yanga chini Mwenyekiti wake DK Mshindo Msolla unaanza kuwapokea nyota wake wapya wa kigeni leo tayari kwa maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga chini ya kocha Mkongoman, Mwinyi Zahera amefanya mabadiliko katika kikosi chake kwa upande wa nyota wa kimataifa kwa lengo la kuongeza ushindani.

Wachezaji hao wataanza kupokelewa kesho na uongozi huo ni pamoja Mnyarwanda, Patrick Sibomana, Sadney Urikhob wa Namibia, Mzambia, Maybin Kalengo, Issa Bigirimana, Mustapha Seleman wote kutoka Burundi.

Yanga inaanza maandalizi ya msimu mpya Julai 7, mwaka huu ikiwa nchini ya kocha msaidizi, Mzambia Noel Mwandila kabla ya Zahera kurejea kutoka mapumzikoni Ufaransa.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Yanga kimesema kuwa wachezaji hao wanaanza kutua tayari kwa ajili ya kuanza maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, alisema: “Ni kweli tunatarajia kuanza kuwapokea wachezaji na mwalimu msaidizi kuanzia leo.”

2 COMMENTS:

  1. Nyie Yanga mtapangaje "Funga Kazi Kusanya Kijiji" ifanyike Taifa kwa Mkapa wakati July 26-28 kwa kalenda ya CAF kutakuwa na mashindano ya CHAN? Hamkuangalia hili? Hamuoni kuwa mtakosa watu au uwanja kuwa na shughuli nyingine ya mchezo baina ya Taifa Stars vs Sudan?? Hebu muwe mnafikiria na kuangalia calendar za Mashindano ya CAF & FIFA Kabla ya kukurupuka na kupanga matukio yenye kuleta mkusanyiko mkubwa wa watu....Fanyeni tafiti kabla ya kupanga tarehe za matukio....! Fanyeni haraka kurekebisha hili....hata timu kuingia Kambini tarehe 7 Julai inaweza ikaathiriwa na hili la CHAN

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic