July 31, 2019



BAADA ya Simba kutoka sare ya kufungana jana bao 1-1 na Orlando Pirates, uongozi wa Simba umetoa tamko kuhusu suala la kudaiwa kubebwa ndani ya ligi.

Simba ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza Agosti 23 na watafungua kazi na JKT Tanzania.

Ofisa Habari wa Simba Haji Manara amesema kuwa kwa aina ya mechi wanazo cheza hakuna haja ya kulalamika kwa sasa.

“Tunacheza mechi ngumu kwa sasa, baadae mtaanza kusema kuwa tunabebwa, wenzenu tunacheza mechi kweli za maandalizi ya msimu ujao,lalamikeni mapema kabla hatujaanza kuwashughulikia,” amesema.

Msimu uliopita Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera alisema kuwa bingwa wa Ligi Kuu Bara alipangwa mapema.


2 COMMENTS:

  1. Ni kweli tupu kuwa timu ambazo Simba imechezanazo huku kambini Afrika Kusini ndizo timu sahihi za kucheza nazo kujitayarisha Kwa msimu ujao Nazo baadhi Zina uwezo wa kushiriki kugombea kombe la klabu bingwa la Afrika

    ReplyDelete
  2. Pia ni kweli tupu kuwa SISIMBWA iliebwa sana msimu uliopitwa TFF iliwasaidia kupanga matokeo kwa ratiba pendeleo, viporo vingi kuachwa na pia penalt nyingine hazikuwa halali bila kusahau maamuzi mabovu toka kwa marefarii...

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic