KIKOSI cha timu ya Tanzania 'Taifa Stars' leo kimelazimisha sare ya bila ya kufungana na timu ya Taifa ya Kenya kwenye mchezo wa kwanza wa kufuzu michuano ya Chan itakayofanyika nchini Camaroon mwaka 2020.
Jitihada za wachezaji wa Stars hazikuzaa matunda na kufanya ubao usome Tanzania 0-0 Kenya mpaka dakika tisini zilipokamilika.
Licha ya Stars, kumiliki mpira kwa asalimia 55 muda wote huku wapinzani wao Kenya wakimiliki mpira kwa asilimia 45.
Mashuti yote matatu yalipigwa langoni hayakuzaa matunda kwani shuti la pili lililopigwa na Iddy Suleiman dakika 58 lilikataliwa na mwamuzi kwa kile alichoeleza kuwa tayari mfungaji alikuwa ameotea huku lile lililopigwa na Salim Aiyee likizaa kona ya saba ambayo nayo haikuzaa matunda licha ya wapinzani Kenya kupiga kona tatu.
Ni mchezaji mmoja tu wa timu ya Taifa, Jonas Mkude alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 70 bado wachezaji walizidi kupambana.
Kazi kubwa imebaki kwa Stars kwenda kumenyana na Kenya ugenini Agosti 4 ili kupata nafasi ya kufuzu michuano hii muhimu.
0 COMMENTS:
Post a Comment