OFISA Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Tido Mhando amesema kuwa ni ngumu kuamini juu ya safari ya wafanyakazi wenzake ambao wamefariki kwa ajali ila kazi ya Mungu haina makosa.
Jana wafanyakazi watano wa Azam Media Group walifariki baaada ya kupata ajali ya gari iliyotokea maeneo ya kati ya Shelui (Mkoani Singida) na Igunga, Tabora.
Waliotangulia mbele za haki ni pamoja na Charles Wandwi, Florence Bitaliho, Said Hassan, Salum Mhando na Silvanus Mhando.
Leo wameagwa na kupumzishwa kwenye makazi yao ya milele na maelfu ya watu ambao wamejitokeza kwenye msiba huu ambao umegusa hisia za watanzania wengi.

0 COMMENTS:
Post a Comment