WILFRED Kidao, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) amesema kuwa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' itakwenda kufanya vema nchini Kenya kwenye mchezo wa marudio.
Stras ililazimisha sare ya bila kufungana na Kenya Uwanja wa Taifa, inakwenda kurudiana na Kenya Agosti 4 na kinachotakiwa ni ushindi ili kufuzu michuano ya Chan.
Kidao amesema:- "Mchezo wa kwanza tulikuwa na nafasi ya kushinda ila ilishindikana kutokana na muda mchache ambao kambi ya timu ya Taifa iliweka chini ya Kocha Ettiene Ndayiragije, kwa sasa kila kitu kinakwenda sawa na ushindi utapatikana.
"Kikosi kimeimarika na kila mmoja anajua jukumu lake hivyo ni muda wetu kuipa sapoti timu yetu ya Taifa kwani nafasi ya ushindi ipo," amesema.
Michuano ya Chan inatarajiwa kufanyika mwaka 2020 nchini Cameroon na njia pekee ya Stars kukata tiketi hiyo ni kushinda mbele ya Kenya.

0 COMMENTS:
Post a Comment