UONGOZI wa Simba umesema kuwa dhamira kubwa ya kuweka kambi nchini Afrika Kusini ni kujiweka sawa kwa ajili ya msimu mpya wa mwaka 2019-20 unaotarajiwa kuanza Agosti 23.
Wakiwa Afrika Kusini wanafanya mazoezi mara mbili kwa siku asubuhi na jioni kujiweka sawa wakiwa maeneo ya Rustenburg, Afrika Kusini.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori amesema kuwa mipango ipo sawa na kambi inaendelea vizuri nchini Afrika Kusini.
0 COMMENTS:
Post a Comment