August 3, 2019


MWINYI Zahera, Kocha Mkuu wa Yanga amethibitisha kuwa ameliondoa jina la kipa wake, Klaus Kindoki katika usajili wao na kumpeleka kwa mkopo Lupopo FC ya DR Kongo.

Kindoki anaondolewa Yanga kwa ajili ya kumpisha mshambuliaji mpya wa timu hiyo Mkongomani, David Molinga Ndama ‘Falcao’ ama mwili jumba akitokea Klabu ya FC Lupopo ya DR Congo kwa mkopo wa mwaka mmoja.

Kipa huyo anatemwa na Yanga kutokana na sheria za usajili za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambazo zinaruhusu wachezaji kumi pekee.

Zahera amesema kuwa maamuzi ya kumuondoa Kindoki siyo ya ghafla na kushtukiza, awali yalikuwepo mazungumzo kati ya Lupopo na kipa huyo kabla ya kumtoa kwa mkopo.
 Zahera amesema kuwa, Kindoki ameondoka baada ya kufikia muafaka mzuri kati yake na viongozi wa Yanga na Lupopo imekukubali kumuachia mshambuliaji huyo kwa ajili ya kukiimarisha kikosi chake.

“Niwaondoe hofu Wanayanga kuwa kabla ya kuja Falcao, nilikuwa nimeshazungumza na Kindoki juu ya yeye kumtoa kwa mkopo kwenda Lupopo aliyokuwa anaichezea awali. 

“Na uzuri yeye mwenyewe Kindoki alikubali kwa moyo mmoja kuondoka kwa mkopo kwenda Lupopo na Falcao kuchukua nafasi yake.

“Hivyo, Kindoki rasmi anakwenda Lupopo kwa mkopo na Falcao anachukua nafasi yake baada ya makubaliano mazuri tuliyoyafikia pande zote mbili Yanga na Lupopo,” amesema Zahera.


11 COMMENTS:

  1. huo ni ukanjanja,hii inaonyesha wazi zahera ni nani pale yanga,lakini ngoja tusubiri kubwa kuliko kutoka kwa hawa maproo wa yanga waliokuja tanzania kutafuta jina na cv kama makambo kisha kuuzwa bila club kunufaika,tusubiri movi la kihindi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tuache ulimbukeni, Simba wamepata nini kwa Okwi na Kotei!? Makambo mkataba ulikuwa umeisha na kazi aliyoifanya ilionekana mlitaka nini cha zaidi!? Hata hiyo 30% ambayo yanga watapata kama akiuzwa kwingine ni favour tu maana hawakumlea.

      Delete
  2. kindoki ameshindwa kutengeneza jina na cv,na hayo ndio masharti ya zahera hivyo lazima aende,kwa akili ya haraka tu je ni kweli FALCAO ni bora kuliko kindoki???kama ndivyo kwanini aje yanga kwa mkopo ikiwa yeye ni proo??akili kichwani kwako.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwan Falcao ni golikipa au mshambuliaji? Unalinganisha visivyolinganishika

      Delete
  3. maana yake ni kwamba wanakuja yanga kutafuta viwango na majina,hebu waende simba wakaone mziki kama hawatapotea mazima kama barafu kwenye jua kali.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Simba ndo nn mbona hueleweki? Usiilinganishe yanga na klabu yoyote nchini. Kuilinganisha yanga na mikia ni kuishushia hadhi na heshima iliyonayo

      Delete
  4. We KEYA mbona unaneng'eneka sana na Yanga??? Tuliza kijambio hicho. Fanya yako achana na habari za Yanga

    ReplyDelete
  5. Na Deo kanda ni proo ama ni nan? Kama ni proo kwann aje kwa mkopo Simba??

    ReplyDelete
    Replies
    1. Deo kanda ni mchezaji mwenye kipaji lakini amekosa nafasi ndani ya timu yake, Falcao yeye ametolewa kwa mkopo kwa kuwa Fc Lupopo wanakiimarisha kikosi chao kwa mujibu wa Zahera.

      Delete
    2. thank you for your asist,be blessed.

      Delete
    3. Mnajitekenya halafu mnacheka wenyewe Deo kanda ana kipaji halafu haohao wakamnunua mess na ambokile!? Ukiwa muongo jitahidi basi kuwa na kumbukumbu!!

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic