August 1, 2019

JUMA Mgunda, Kaimu Kocha Msaidizi wa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' amesema kuwa kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Ibrahim Ajib anasumbuliwa na majeruhi kwa sasa.

Mgunda amesema kuwa kwa sasa kikosi kinafanyia kazi makosa waliyofanya awali kabla ya kurudiana na Kenya Agosti 4 nchini Kenya.

"Ibrahim Ajib kwa sasa yupo kwenye uangalizi wa madaktari baada ya kupata maumivu ya mguu kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Kenya.

"Wengine wote wapo sawa na wanaendelea kujipanga kwa ajili ya mchezo wetu wa marudio, tunayafanyia kazi makosa yetu ya mchezo wa kwanza ili kupata matokeo chanya," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic